AJTC

Monday 26 December 2016

mapambo ya nyumba unaonaa

Mpangilio ndani ya nyumba...


Images courtesy apartment therapy
Mpangilio mzuri ndani ya nyumba huongeza nafasi na hupendezesha nyumba. Mfano ni hizi bookcase (zinaitwa expedit kutoka IKEA) zinaweka vizuri mpangilio . Picha ya hapo juu ili kupendezesha karatasi za ukutani (wall paper) imewekwa nyuma ili kuongeza mvuto. Panga vizuri ndani ya nyumba utafurahi na kupapenda unapoishi.Enjoy!


JIONEE MAPAMBO YA KIAFRIKA YANAVYOPAMBA NYUMBA ZETU ZA KISASA

Na
 Hiki ni chumba kimoja, kwa wale wanaokaa chumba kimoja basi huu ni mfano wa kuigwa......
 Sehemu za chakula unaweza kuweka kabati dogo na mapambo kiasi, sio lazima ukaweka kabati la vyombo, una jiko kubwa basi, weka vyombo jikoni na kwa mpangilio mzuri
 Sebule ilivyotulia, hakuna mambo mengi, ama picha nyingi ukutani......
 Picha zinahitaji umakini, kwanza kwenye kuchagua, na kutundika ukutani, ili kuleta muonekano mzuri...
Waweza changanya fanicha kama tuonavyo.......rangi pia z a mito ya mapambo. 
 
 

MAPAMBO YA KUMBI ZA SHEREHE





Hizi picha zaonyesha mojawapo ya namna ya kupamba kumbi za sherehe mbalimbali. Nitawaletea picha na mawasiliano ya moja kwa moja ya wahusika wanaoweza kukupambia sherehe yako kwa staili na urembo unaopenda kadiri ya nguo mtakazovaa n.k. 
 
 

JINSI YA KUPUNGUZA MAFUTA MWILINI

Habarini ya leo nduguzanguni
leo hii napenda kuwaeleza dawa au juice mpya kwa ajili ya kupunguza mafuta mwilini.
hii juice si kama inapunguza mafuta mwilini tu bali pia kama umekosa kwenda haja
kubwa badala ya kutumia mapapai pia unaweza kutumia juice hii

vitu vinavyohitajika katika kutengeneza juice hii
1. ukwaju kilo moja
2. maji safi na salama lita 3.
3. Asali kiasi tu (hii inatumika badala ya sukari).

JINSI YA KUTENGENEZA.
Chukua ukwaju na weka katika chombo kisafi kikubwa cha kuweza kutosha kutengenezea hiyo juice yako.
weka maji lita 2
acha uloane kwa mda wa masaa manne hadi matano
nawa mikono yako
fikicha ule ukwaju na utoe mapeke.
chukua lita moja ya maji uliyobakiza na uweke tena kwenye juice yako ili ikamilike lita 3.
chuja juice yako
ukiwa umeshachuja kwa umakini chukua asali na uweke kisha koroga kwa mda mrefu kama dk 5 hadi 10
ili juice yako ichanganyike vizuri na asali.
kipimo cha asali utaangalia mwenyewe kama inatosha au la kwani ni badala ya sukari kwa hiyo unaweza kukadiria.
ikishakuwa tayari unaweza weka kwenye kidumu au kwenye chombo unachoona wewe kinafaa kisha weka kwenye fridge ipoe kidogo.
tumia grass moja asubuhi na grass moja jioni kabla ya kulala.

TAHADHARI:. baada ya kunywa hii juice utaharisha sana tena sana ila tumbo halitakuuma na huwezi pata mazara yeyote zaidi ya kuharisha. kwa hiyo ukijua umetumia hii juice jaribu kukaa karibu na toilet mda wote na tishu ziwepo kwa wingi. maana ni full maharibiko katika tumbo lakini ni dawa nzuri sana sana.
 
 

NJIA KUMI KUSAIDIA KUPUNGUZA UNENE

Muda mrefu wasomaji kadhaa wameniomba nifafanue mada hii.  Ni mada muhimu sana. Wastani wa maisha ya Mtanzania ( na Waafrika wengi) hata wale waliosoma au wanaojiweza kiuchumi ni miaka 40-50. Kati ya sababu kuu zinazopunguza uhai wetu ni afya, unene na kutojua kujiangalia vyema.
Mazoezini na baiskeli nje ya mji wa Bournemouth, kusini ya Uingereza, 2008- Picha na Z. Macha
1-ULAJI
Ipo mifumo miwili ya kula. Chakula unachokula na namna unavyokila.
Unavyokula.
-Kuna kula vyakula vidogo vidogo vyenye madini, vitamini, mafuta nk mara nyingi kwa siku; au kula milo michache (mmoja au miwili) mikubwa ili kujaza tumbo. Ulaji mdogo mdogo husaidia afya na kuingia mwilini vyema kuliko ulaji mkubwa wa mara chache. Tumbo lina musuli zinazofanya kazi kama mashine au mnyama. Gari likijaa sana hupata taabu kwenda. Punda hivyo hivyo. Ulaji mdogo mdogo unaosambazwa mara kadhaa kwa siku  ni bora maana mwili unachambua kila kitu kwa wepesi na haraka. Unapokula milo michache mikubwa unapalilia zaidi mafuta mwili.
(PENDEKEZO la kwanza.  Asubuhi, kunywa maji kwanza, matunda, kisha ndiyo chai na vitu vingine kama mkate au maandazi…)
-Wapo wanaodai kwamba wanakula matunda na mboga.
Tatizo ni kwamba mipangilio  yao huwa ya makosa. Mathalan wengi hula matunda baada ya chakula. Vimeng’enya  chakula (enzymes) tumboni hufanya kazi namna tofauti. Mathalan vile vinavyonyambua matunda ni tofauti na vinavyomeng’enya vitu vigumu zaidi kama nyama au wanga. Matunda hunyambuliwa haraka zaidi kuliko vyakula vingine. Hivyo ni bora kula matunda dakika10-20 kabla ya chakula. Ukila baadaye matunda hugeuzwa aina fulani ya pombe (fermented food) inayoelea tu juu ya chakula na kubakia kitu kingine badala ya kuingizwa haraka ndani ya damu kupitia utumbo mdogo, uwengu, moyo, ini, nk.
Tatizo jingine ni kupika sana mboga hadi zikapoteza nguvu.
-Mseto wa vyakula pia ni muhimu. Kwa mfano vyakula vyenye uchachu (“acid”) na vile vinavyomumunyuka haraka (“alkaline”) havitakiwi viliwe pamoja. Mfano ni matunda. Matunda chachu kama machungwa, mananasi na maembe yatakiwa yawe pamoja; na yale laini zaidi:  ndizi mbivu, matikiti maji, mapapai, matufaha, nk yaende kivyake, maana yana mfumo tofauti, wa kumeng’enywa.
Mpishi Patrick Maka ( katikati, akiwa na wenzake kazini Dar) ni kati ya wapishi wa Kitanzania wanaopigania sana ulaji wa chakula bora
Hali hiyo pia iko katika nyama. Nyama nyeupe (ndege na samaki) tofauti na nyama nyekundu (ng’ombe, kondoo, nk) ziliwe tofauti.
Chakula unachokula
Waafrika  hatuna tabia ya kula mboga mboga mbichi. Tunafuata ladha na mazoea kuliko thamani.
Bara letu lina mboga na vyakula bora kuliko bara lolote duniani lakini sisi tunakufa mapema na kwa utapia mlo kuliko wale wanaotoka nchi kame. Ulaya nzima imejazana mboga mboga zinazoagizwa toka Afrika. Kenya na Tanzania zinauza mboga za maharagwe mabichi (green beans), matunda toka Afrika Kusini na Ivory Coast; nk. Waafrika tunapenda kujaza matumbo. Unene umekithiri hata wale walio matajiri waliosoma bado wanakufa kwa kisukari shauri ya kutokula mboga mbichi.
Ulaji wa mboga mbichi ni upi?
Ni mathalani ulaji wa salad. Tanzania tunaita kachumbari. Lakini si lazima iwe kachumbari ya nyanya, vitunguu na chumvi tu. Waweza kuchanganya matango, nyanya kwa maparachichi; au vitunguu saumu, giligilani na karote. Huu mseto wa mboga mbichi ni mzuri ukienda na chakula chenye nyama za minofu na wanga (ugali, wali, ndizi za kupika nk). Ulaji wa wanga asubuhi, mchana na jioni kila siku huchangia sana katika unene.
(PENDEKEZO LA 2. Ugali kwa samaki; mboga ya majani ya matango kwa nyanya. Usiweke chumvi kwenye hiyo mboga mbichi ya majani.)
Majani na mimea yamezingirwa na barafu Ulaya- vyakula vingi vya watu hawa huagiziwa na kutegemewa Afrika. Lakini wanakula vizuri kutuzidi. Kwanini? Picha na F. Macha
2-UNYWAJI  MAJI
Waafrika hatunywi maji, hasa wanawake. Wanaokunywa maji zaidi ni wacheza michezo. Wengi wetu hunywa zaidi soda (vinywaji baridi kama Cocacola, Pepsi, Mirinda ,Tangawizi  na gesi za kisasa kama Red Bull) zilizojaa gesi inayoleta vidonda tumboni; na chai. Kuliko maji. Na maji haya hutakiwa  dakika 10-20 kabla ya chakula au nusu saa kuendelea baada ya chakula. Ukila  chakula huku unasakatia maji huimanisha mtu una kiu. Ulaji chakula na unywaji maji ni vitu viwili tofauti. Ila utawaona watu wanakula huku wakibugia maji. Unapokula chakula huku unabugia maji unapunguza nguvu za chakula, unajaza tumbo maji na kuchelewesha mmeng’enyo wa chakula (digestion).
Chakula kisipomeng’enywa vizuri kinaketi tu tumboni. Matokeo wengi wetu tuna  matumbo makubwa. Kama hufanyi mazoezi lile tumbo linakwenda pembeni (chini ya mbavu) hasa kwa watu wa makamo linaleta maradhi kama kisukari, kiungulia, kuvimbiwa, uyabisi wa tumbo, nk. Kizungu huitwa “love handles.”…
Farasi ni mnyama asiyeliwa ovyo Uingereza; hufugwa tu kwa kazi na michezo. Ipo hoteli moja Scotland imeanza kupika nyama yake kwa chips. Imeandamwa sana na "wapinzani wa kula nyama" wa Kitasha... (Picha na F. Macha)
3-SUALA LA UMENG’ENYAJI
Chakula huanza kumeng’enywa au kusagwa (kwa lugha iliyozoeleka) mdomoni. Mate yako mdomoni ni chanzo cha uchambuaji chakula. Unapobugia chakula bila kutafuna sawasawa unasababisha mambo mawili. Moja chakula kutochambuliwa vizuri, pili chakula kwenda kukaa tu tumboni, au kama kikipita hakisaidii lolote mwilini. Utafunaji wa taratibu husaidia umeng’enyaji. Chakula kinapofika tumboni hukaa pale dakika ishirini. Hapo huchanganywa na asidi (ya manjano iitwayo Hydrochloric) inayokibadilisha tayari kupelekwa utumbo mkubwa, kupitia kongosho. Kule uchafu utapelekwa chini na rutuba kusafirishwa na utumbo mdogo kuelekea katika uwengu, moyo. Moyo utadunda chakula kilichoshageuzwa damu kuelekea mwilini kufanya kazi na akiba hubakishwa katika ini.
Sasa kama usipotafuna vizuri, ukila huku unakunywa sana maji au vinywaji vingine chakula hakimeng’enywi vizuri. Ndiyo maana unawaona watu wengine wanakula sana lakini hawana afya. Wanaugua ovyo ovyo, wanatoka jasho ovyo, wanajamba ovyo, wana matumbo makubwa, wanavimbiwa, wanakaa siku nyingi bila kwenda choo (inatakiwa mtu kwenda haja kubwa mara moja au mbili kwa siku) nk.
Misitu na hewa safi ya mimea- (Picha na F. Macha)
4-ULAJI WA VYAKULA VYA MAFUTA
Mafuta ni suala muhimu sana mwilini. Ila ulaji wake shurti uwe wa mpangilio. Yaani unaowiana. Lazima mtu uwe na wastani mzuri wa vyakula vya nguvu, yaani “wanga” (ugali, ndizi, wali, viazi mbalimbali, mikate, mahindi, nk), ujenzi yaani “protini” (mboga na nyama), “madini” (mbegu mbegu mbichi si za kukaanga sana na chumvi) na “vitamini” (matunda, maziwa, mayai, nk).
Waafrika tunapenda nyama. Nyama ni muhimu sana maana ina madini aina ya chuma (nyama nyekundu) protini,nguvu na mafuta. Ila mafuta yaliyoko katika nyama mara nyingi si mazuri shauri hayatoki, huganda. Chukua nyama ya kuku na samaki ambayo huwa na ngozi. Wengi wetu hupenda sana kula ile ngozi ya wanyama hawa kwa kuwa tamu. Lakini haya ni mafuta mabaya.
Mafuta ya samaki lakini ni mazuri. Samaki anayo mafuta ya Omega-3 ambayo husaidia mwili na kinga maradhi mwilini.
Tunapokula nyama choma au ya kukaanga, lazima tule pia mboga za majani (mbichi) na si vizuri kula nyama kila siku. Kama huwezi kukaa bila nyama kila siku, fanya mazoezi ya mwili.
PENDEKEZO LA 3- Kula mbegu mbegu za korosho, karanga au mlozi (ziwe mbichi badala ya kukaanga na chumvi) kati kati ya siku. Haya ni mafuta yenye rutuba mwilini kuliko nyama za mafuta.
Chips za Magimbi zilizopikwa na mpishi Mtanzania Miriam Rose : http://www.tasteoftanzania.com
Chips za Magimbi zilizopikwa na kuonyeshwa ndani ya tovuti ya Miriam Rose ,  dada wa Kibongo anayetukuza mapishi ya Kitanzania duniani. Habari zaidi tembelea : http://www.tasteoftanzania.com
5-MAZOEZI YA MWILI NA VIUNGO
Mazoezi ni mfalme wa kupunguza unene.
Ukiwauliza wengi watakuambia wanafanya kazi ngumu za sulubu (wanachuruzikwa jasho) kwa hiyo hayo ni mazoezi. Ila kazi na mazoezi ni vitu viwili tofauti. Ingekuwa kufanya kazi ni mazoezi basi kusingekuwa na wastani mfupi wa maisha kwa maskini hasa sisi Waafrika.
Wengine watadai kwamba walipokuwa wadogo shuleni walifanya mazoezi sasa wamekuwa watu wazima (miaka 40 kuendelea) kwamba eti mazoezi ni suala la ujana; kumbe kadri unavyokuwa ki umri ndivyo kadri unavyotakiwa kufanya mazoezi na kujitazama zaidi kiafya.
Watazame Wachina na Wajapani wanavyoishi maisha marefu.
Mazoezi ni shughuli inayokufanya kwanza uheme (mapafu na moyo kwenda kasi), viungo na mifupa kujinyoosha (stretching), kutoka jasho na usafishaji wa damu. Mazoezi yanayosaidia haya ni pamoja na kutembea kasi, kukimbia, kuogelea, michezo mbalimbali ya riadha (kama mpira wa miguu, nyavu, kikapu, mikono, nk); michezo ya kupigana na kujilinda yaani masho ati(karate, kung fu, judo, capoeira, krav maga, jiu jitsu, systema, kickboxing, thai boxing, kempo, kalari payatu, aikido, nk) …
Ni muhimu mwanadamu ufanye mazoezi makali ya viungo mara mbili tatu kwa juma. Si vizuri kufanya kila siku kwani musuli na mishipa inahitaji kupumzika na kukua.
Kama unapenda kuinua vyuma lazima uwe na mwalimu wa kukuelekeza; na si vizuri kufanya kila siku.  Wastani wa mara mbili tatu kwa juma inatosha kabisa.
Mdau wa Kitoto naikabili bahari shakiri na baridi sana ya English Channel. Kuogelea ni moja ya tizi bab kubwa lisilohitaji kingine bali mwili wako...maji bure asilia ya Muumba al Dunia. (Picha na A. Macha)
6-UPO UFANYAJI MAZOEZI WA AINA MBILI
Mazoezi ya nguvu ya kuhema niliyotaja hapo juu (cardio-vascular) na yale laini ya kujinyoosha yaani ambayo hutumia zaidi nguvu za ndani na pumzi. Haya ya pili ni kama Yoga (India) , Tai Chi Chuan (China) na aina mpya mazoezi iliyoanza Majuu miaka ya karibuni yaani Pilates (hutamkwa hivyo hivyo ilivyoandikwa Pilates). Haya laini yanawafaa zaidi watu wazima na nchini China na Japan mathalan utawakuta wazee wa miaka 80 hadi 90 bado wanayafanya. Husaidia moyo, damu na akili.
Michezo na mazoezi ya mwili ni njia kuu ya kupunguza unene, kurefusha maisha, kuchangamsha ubongo, kupunguza ulevi, uvutaji sigara, dawa za kulevya, tabia mbaya za uvivu, ugomvi, nk.  Mataifa yenye watu wanaofanya mazoezi kama Japan, Brazili, India, China nk  huwa na wachapa kazi wengi na wananchi wanaoipenda jamii yao.
Chakula cha wanga kwa wingi kilichozoeleka sana Afrika ni kitamu; ila kinakosa mboga mbichi za majani, yaani Saladi- (Picha na F Macha)
7-KULA SANA CHUMVI SI VIZURI
Ulaji chumvi mwingi hutokana na suala la ladha. Kisayansi vyakula  vyote vina chumvi asilia sema tu tumezoea kuongezea madini hii iitwayo Sodium. Sodium inachangia sana kufupisha maisha. Huifanya mishipa ya damu ichoke; ni kama bomba lolote la maji ukilitazama baadaye hugeuka rangi kutokana na yale maji kupita pale kila siku.
Kwa wale tunaoishi nchi za joto na kutoka sana jasho kula chumvi ni muhimu. Ila tatizo letu ni kwamba hatunywi maji ya kutosha. Mtu ukiwa na kiu unakunywa soda au kinywaji cha sukari; inakuwa kama unaendelea kuutesa mwili. Kwa vipi? Mishipa inayopitisha damu mwilini badala ya kusaidiwa kwa maji inawekewa kazi zaidi ya kusafisha sukari na chumvi. Ndiyo maana vifo vingi vinatokea mapema; wastani wetu wa maisha haupiti miaka 50.
Utafiti uliofanywa chuo kikuu cha California, Marekani mwanzoni mwa 2010, umethitibisha kwamba vifo vingi duniani husababishwa na maradhi ya moyo na saratani ambavyo hutokana na uvutaji sigara, unene, ulevi na ulaji sana wa chumvi na sukari. Tukipunguza ulaji wa chumvi tunasaidia pia kupunguza maradhi ya moyo, utafiti unasema.
Mabasi ya ghorofa daraja mashuhuri la Tower Hill, London. Asilia kubwa ya wakazi hapa wanahusudu sana mazoezi shauri mji umebanana sana na hewa si safi. Taswira ilipigwa na mpiga picha Mike Nicholas, baharia wa Kibongo mkazi, Denmark, alipotembelea jiji hili la nne duniani kwa gharama, karibuni .
8-TAFITI ZA VYUO KADHAA ULIMWNGUNI KUHUSIANA NA AFYA
-Jarida la Kimarekani la sayansi lilieleza mwaka jana kwamba utapunguza ugonjwa wa moyo (ambao husababishwa na unene , wasiwasi na purukshani) kwa asilia mia 42 kama utakula matunda na mboga za majani peke yake kila siku, juu ya msosi wa kawaida.
(PENDEKEZO LA KULA- Na 4- Kula mlo wako. Baada ya saa mbili au tatu, sakatia tunda au matunda; baada ya mlo mwingine, kula sahani ya mseto wa mboga mbichi kama karote na matango. Utaona tofauti ya afya, ngozi, wajihi, kinyesi, usingizi, nk. Kidesturi tumezoea kunywa chai au soda za sukari sukari na gesi kati kati nya milo badala ya matunda na mboga mbichi za majani).
-Utafiti uliofanywa na wanasayansi  chuo kikuu cha South Carolina mwanzo wa mwaka 2010 kuhusu faida za kuogelea.
Zoezi la kuogelea  lina faida zaidi ya kukimbia au kutembea kwa vile huchanganya mazoezi makali na pumzi, kusaidia mapafu na moyo. Utafiti ulithibitisha kuogelea hupunguza hatari za kifo kwa asili mia hamsini.
-Utafiti wa jarida la chuo cha uganga Ulaya umeeleza (desemba 2009) kwamba kulala nusu saa kila mchana (“nap”) husaidia  kupunguza ugonjwa wa moyo kwa asilimia 37.
-Uchunguzi wa chuo cha michezo cha Hispania mwanzoni mwa 2010 umethibitisha kwamba ukikimbia mara tatu kwa juma (jogging) unaongeza nyege mwilini kwa asili mia 75. Hasa kwa watu wa makamo mnaoanza kupoteza nguvu za urijali.
-Uchunguzi chuo kikuu cha Leeds, Uingereza  mwanzoni mwa 2010 umeonyesha unapotembea kwa miguu, ukikwepa barabara kubwa zisisokuwa na mioshi ya magari (pollution) unapunguza matatizo ya maradhi ya hewa chafu kama pumu, mapafu na appendix.
-Uchunguzi wa chuo kikuu cha Texas mwaka 2010 umegundua kwamba  kula tunda la divai nyekundu mara kwa mara husaidia kupunguza  kupata ugonjwa wa kisukari.
-Hapo hapo tunaelezwa kwamba watu weusi na bara la Asia wanakumbwa zaidi na ugonjwa wa kisukari kutokana na vinywaji vya sukari sukari na gesi (fizzy drinks). Ukinywa kiasi cha miligramu 300 za vinywaji hivi (Cocacola, Red Bull, Fanta, nk)  kwa siku unajitahadharisha kupata kisukari.
Njiwa London, mtaa wa Westbourne Park. Huruhusiwi kisheria kumpiga manati, kumuua au kumfanya ndege huyu kitoweio nchi hii. (Picha na F. Macha)
9-KUFUNGA
Neno kufunga linatambuliwa rasmi kuhusiana na Waislamu (mwezi Ramadhani) au Wakristo (Lenti nk). Ufungaji huo una masharti mengine ya kidini tofauti na haya ya kiafya.
Mathalani wafungaji  hawa hula chakula kingi usiku; ukihesabu wanafunga wastani wa saa 12 tu. Kawaida ukitaka virusi na takataka nyingine mwilini zitoweke, au viungo vipumzike wahitaji saa 20 kuendelea.
Ufungaji ninaouongelea ni ufungaji wa kutokula kabisa kwa saa 24, 36 hadi 48 kuendelea…
Ufungaji ni nini?
Kama mashine yeyote mwili wa mwanadamu unahitaji kupumzika na kujisafisha. Hata tukiwa tumelala bado viungo mbalimbali mwilini vinafanya kazi. Kwa hiyo faida ya kwanza kabisa ya kufunga ni kuupumzisha mwili kama mfanyakazi yeyote anapokwenda likizo.
Faida ya pili ya kufunga ni kusafisha mwili kutokana na uchafu ambao haukutoka (kinyesi hakitoi mabaki yote toka utumbo mkubwa), dawa na takataka za mazingira tunayoyavutia hewa, virusi au kuyanywa katika maji na vyakula mbalimbali na pia uchafu wa hisia, yaani hasira, huzuni, nk.
Kuna ufungaji wa aina mbalimbali.
1-Kufunga kwa kunywa maji tu, saa 24 kuendelea…
2-Kufunga kwa kutokunywa maji au kula chochote, saa 24 kuendelea…
3-Kufunga kwa kula tu matunda au mboga zilizopondwa kama karote, matango nk, saa 24 kuendelea…
Ufungaji huu unatakiwa ufanywe kwa mpangilio. Kitu muhimu si tu kufunga bali NAMNA unavyofungua. Ukianza kula tena, unaanza taratibu. Kawaida ni vizuri kuanza na maji, kikombe au bilauri ya kwanza taratibu. Subiri tena nusu saa, bilauri nyingine, halafu hadi ya tatu, halafu ndiyo matunda yasiyo ya chachu, na kadhalika. Kuanza kufungua kwa kunywa chai ya maziwa, uji au vyakula vingine vya wanga hakusadii sana mfungo huu.
Maana lengo lake ni kusafisha mwili.
PENDEKEZO LA 5- Kwa wenye imani za kidini. Unaweza pia kufunga hivi ukawa pia unasali au kuvaa mavazi yanayokufanya mtu wa amani. Ukifanya hivi unajitakasa kimwili na kiroho. Si lazima ungojee ile miezi ya kufunga na wengine.
10-USINGAJI
Usingaji au masaji ni njia nzuri sana ya kupunguza unene. Ikiwa unaangalia namna unavyokula, unafanya mazoezi na kusingwa mara moja au mbili kwa mwezi unaupalilia mwili vizuri. Nini faida ya usingaji? Kusinga husaidia ngozi, mishipa ya damu na sura nzima ya mwili na taswira yako mwanadamu. Wengi wetu tunaposikia neno kusinga tunafikiria usingaji wa mapenzi. Hivi ni vitu viwili tofauti kwani usingaji wa mapenzi unaimanisha mahusiano ya kihisia.
Kifupi mwanadamu unatakiwa uwe unautunza na kuungalia mwili wako kama nyumba au hekalu lako. Wengi wetu tunaoga, tunajipaka marashi, tunasuka, tunanyoa nywele au ndevu; lakini miili yetu kiundani inaoza taratibu…
Miti na maua asilia ya Mola nje ya Imperial College, London. Hiki ni kati ya vyuo vikubwa vya kisayansi, duniani. Hapa miaka mingi wataalamu wamekuwa wakitafiti dawa ya kupambana na mbu anayeeneza Malaria, Afrika. (Picha na rich voice)
Kama alivyosema mpiganaji, msanii, mwanafalsafa, mwigizaji, mwandishi mashuhuri marehemu Bruce Lee katika shairi  lake Mazingira Yako Kimya (toka kitabu “Msanii wa Maisha”, Turtle Publishing, 2001):


RANGI ZA NYUMBA ZINAZOROCK KWA SASA

Ukuaji wa teknolojia umeongeza kwa kasi mabadiliko katika ujenzi wa nyumba zetu.miaka ya nyuma wengi walipaka rangi cream au nyeupe kwa ndani tofauti na sikuhz ambapo rangi huchanganywa kwa teknolojia ya kisasa ya kutumia compyuta na kupelekea kuongeza uwigo mpana wa uchaguzi wa rangi za kupaka ndani na nje ya nyumba zetu.
Muhimu kuzingatia ni kuwa rangi hizi znazoshine kwasana mfano orange, zinapendeza kuwekwa kwa ukuta mmoja tu kwa ndani na kwingne zinabaki rangi zisizo na kelele yaani zilizotulia.Zaid kwenye vyumba vya watoto wa kiume wengi hupendelea blue wakati kwa wakike pink,purple na orange au green hupendeza zaid.
Kama ilivyo ada tunakupa mifano kwa picha na itakusaidia kukupa maamuzi pale utakapohitaji kununua rangi za nyumva yako.Zaidi sikuhiz rangi hata gypsum zinapendeza ukiweka tofauti na nyeupe kama wengi walivyozoea.(picha ya rangi za gypsum toka kwa mdau wangu wa ujenzi zone)

Saturday 24 December 2016

UREMBO DADA WEWE WA MAVAZI NA WA MWILI KIUJUMLA.

Mavazi na Urembo


image
Pochi ni sehemu muhimu sana katika maisha ya mwanamke. Pochi zipo za aina, rangi, ukubwa na matumizi mbali mbali. Ni nadra sana kukutana na binti au mama anayetembea bila pochi, na kwa wengine maisha yao yote wanatembea nayo kwenye pochi.
Kuna vitu muhimu ambavyo ni lazima kila mwanamke akumbuke kutembea navyo kwenye pochi, na kuna vingine ni vyema kuwa navyo lakini sio lazima.
Muhimu
1. Pini
2. Sindano na uzi
3. Vifungo
4. Dawa yoyote ambayo unaitumia na kuihitaji
5. Kitambulisho
6. Pedi
7. Kalamu na notebook

Ukipenda
1. Perfume
2. Lip shiner / lip stick
3. Poda
4. Kitana
5. Khanga / mtandio
6. Kadi ya benki
7. Sandals kama unavaa viatu virefu

Mara nyingi wanawake tumekuwa tukijichukia na kujiona si wazuri wala hatupendezi kwa kuangalia muonekano wa nje. Unajiangalia na kujilinganisha na wengine na kuishia kuona mabaya (usiyoyapenda) na kuacha kuona jinsi Mungu alivyokuumba vyema na kukubariki. Utaona kuwa hauna nywele nzuri kama fulani, umenenepa/ kukonda sana, hauna elimu kama wengine, haujaolewa na mengine mengi.
Tambua hakuna mwanadamu aliye mkamilifu bali Yesu Kristo Bwana wetu ndiye atukamilishaye. Hivyo ulivyo ni wa thamani sana mbele zake na anakuhitaji uache kuangalia madhaifu yako bali umwangalie yeye ili aweze kukutumia. Jenga tabia ya kuhesabu baraka zako kila siku na utaona jinsi maisha yako yatakavyo badilika. Jione vile Mungu anavyokuona na acha kutumia vipimo vya wanadamu kutambua thamani yako.
Hivyo ulivyo Mungu anataka kukutumia, kwa elimu uliyonayo, kazi uliyonayo, nafasi yako hiyo hiyo uliyonayo, Mungu anakuhitaji. Unaweza kudhani kuwa ungekuwa na elimu zaidi, nafasi kubwa zaidi kwenye jamii, umeolewa, unakarama kama ya fulani basi ungemtumikia Mungu. Ukweli ni kwamba hivyo ulivyo unahitajika shambani mwa BWANA, kwa karama aliyokupa (kila mmoja wetu amepewa, nitafundisha juu ya hili siku zijazo). Anza sasa kumtumikia Mungu na utaona jinsi gani utabarikiwa na kuinuliwa zaidi na zaidi.
1 Korintho 15:10 Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si bure, bali nalizidi sana kufanya kazi kupita wao wote; wala si mimi, bali ni neema ya Mungu pamoja nami.”

1Samweli 16:7 Lakini BWANA akamwambia Samweli, usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. BWANA haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje,bali BWANA hutazama moyo.
Mungu pekee ndiye anayeweza kuuona moyo wa mwanadamu, mwanadamu hawezi kuona moyo hivyo yeye yupata majiby yake pale anapoangalia mwonekano wa nje. Kutokana na hili basi ni vema wanawake wa kikristo tukawa na muonekano mzuri ili uwe ushuhuda mwema kwa wale wanaotutazama. Moyo mnyenyekevu na mwema huonekana katika muonekano wa nje, ni vyema tukajitahidi kuvaa vizuri, nadhifu na maridadi bila makwazo wala kujishushia thamani.
Muonekano mzuri ni muhimu sababu wewe ni kielelezo kwao waaminio na kwa wale wasioamini na kwa familia yako pia. Kwa wale walioolewa hakikisha muonekano wako haumfanyi mume wako akakosa heshima, vaa vile mume wako anavyopendezwa kuliko kuvaa ili kuwapendeza watu wengune.
2 Korinto 11:7b..Lakini mwanamke ni utukufu wa mwanamume.
Pia kumbuka kuwa muonekano wako unaonyesha jinsi ulivyo, kama upo rafu rafu basi inaonyesha kuwa hata katika mambo yako mengine haujali, haipendezi mdada kwa na nywele zimefumuka au kuchakaa bila kuzitengeneza vizuri, au kuvaa nguo inayoonyesha sehemu kubwa ya mwili wako mfano kifua, mgongo au mapaja. Kwanza unajivunjia heshima na kumdharaulisha Mungu wako wa wale wanaokuona.
Vaa nguo inayokutosha vizuri, sio kubwa sana sio ndogo sana, hakikisha nguo ipo katika hali nzuri, sio unavaa sketi zipu imefungwa na pini au blauzi isiyo na baadhi ya vifungo. Pia ujue nguo ipi ni ya kuvaa mahali gani na kwa wakati gani, sio nguo ya kwenye sherehe ya usiku wewe unaivaa kanisani. Jitahidi kuuweka mwili wako katika hali nzuri, usiwe na harufu ya jasho wala nywele zisiwe na harufu yoyote mbaya. Tunza mwili wako maana ni hekalu la Roho mtakatifu. Jipende kwanza mwenyewe ili watu wengine nao waweze kupendezwa nawe.
Ubarikiwe.

Mikono ni mojawapo ya sehemu muhimu katika mwili wa mwanamke. Mikono hutumika kufanya shughuli zote za nyumbani kuanzia kupika, usafi, malezi n.k na isipotunzwa vizuri ni rahisi sana kuharibika na kupoteza mvuto wake wa asili. Urembo wa mikono sio lazima ufanyike saluni au kwa wataalamu, wewe mwenyewe unaweza kufanya hivyo kwa muda wako kwa gharama nafuu.
Vitu Vinavyohitajika
  • Pamba ya kutolea rangi kama umepaka rangi
  • Dawa ya kutolea rangi
  • Mashine ya kukatia kucha au mkasi mdogo
  • Tupa ya kucha (Nail file)
  • Brash ndogo ya mikono
  • Sabuni ya kunawia
  • Rangi ya kucha kama utapendelea
1.Kwa kutumia pamba na dawa ya kutolea rangi toa rangi yote kwenye kucha na hakikisha imetoka kabisa.
2. Kata kucha zako kwa urefu unaoutaka kwa kutumia ‘nail cutter’ au mkasi mdogo.
3. Lainisha ncha za kucha zako kwa kutumia tupa ya kucha, hakikisha unazisugua kuelekea upande mmoja ili kuepuka kucha kuvunjia. Kusugua kwa kwenda mbele na nyuma husababisha kucha kuvunjika upesi.
4. Kwa kutumia maji ya uvuguvugu na sabuni laini pamoja na brashi ndogo ya mikono, osha mikono yako vizuri na kuisugua  hasa sehemu za kucha.
5. Kausha mikono yako vizuri kisha paka losheni, hakikisha umepaka hadi kati kati ya vidole.
6. Kama utahitaji kupaka rangi, chukua pamba na remover na kutoa mafuta kwenye kucha zako kisha anza kwa kupaka rangi ya maji mpako mmoja na ikisha kauka ndipo upake rangi uliyoikusudia. Paka mpako wa kwanza acha ikauke kisha paka mpako wa pili na ukishakauka malizia na rangi ya maji ili kung’arisha na kuleta mvuto zaidi.
Tip: Kama kucha zako zimebadilika rangi kutokana na kupaka rangi mara kwa mara, loweka mikono yako kwenye maji yenye limao kwa dakika 5.
Kama hauna tupa ya kucha unaweza kutumia kiberiti ule upande wenye baruti.

Urembo na Mapambo
  • Bangili, hereni na mikufu unayoitumia mara kwa mara vinafaa vitundikwe kwenye stand maalumu mahali panapofikika kiurahisi mfano juu ya dressing table ili iwe rahisi kuvichukua na kutumia kila unapohitaji na kuzuia visishikane na hatimaye kuharibika.
  • Vito vya thamani viwekwe mahali salama kwenye container au box dogo zikizungushiwa kitambaa laini au sponji ili kuhifadhi thamani na mng’ao wake.
  • Hifadhi vitu vya aina moja pamoja, mfano dhahabu, silva, plastic, shanga, n.k ili iwe rahisi kujua kitu fulani kipo wapi kinapojitajika.
  • Hakikisha mikufu yote imefungwa vyema kuepuka kushikana na hatimaye kukatika.
Viatu
  • Viatu unavyovivaa mara kwa mara viweke kwenye ‘shoe rack’ mahali ambapo ni rahisi kuonekana kama ni kwenye korido au sehemu  yoyote rahisi kufikika.
  • Vipange viatu vyako kwenye shoe rack kufuatana na rangi, urefu wa kisigino, aina ya kiatu au matumizi.
  • Hakikisha viatu vyako ni vikavu na safi kabla ya kivihifadhi na hifadhi sehemu kavu isiyo na maji au unyevu.
  • Viatu ambavyo havivaliwi mara kwa mara kama vile vya kuvaa kwenye matukio maalinu ya usiku ni vyema vikihifadhiwa kwenye sehemu ya chini ya kabati.
Pochi
  • kama viatu pochi pia zinapendeza na pia kukusaidia kuokoa muda zikihifadhiwa kwa ukubwa, rangi, aina au matumizi.
  • Pochi unazotumia mara kwa mara weka kwenye stand maalumu na nyingine unaweza weka kabatini ili kupunguza wingi wa vitu kutundikwa kila mahali.
  • Pochi ndogo na wallet ziwekwe pamoja ndani ya droo au pochi kubwa ili kuepuka kupotelea ndani ya nguo au pochi nyingine.
Shalom
Dada Maria aliulizia kuhusu maternity wear ambazo zinaweza kuvaliwa ofisini na ukaonekana vizuri. Hapa kuna baadhi ya nguo ambazo zinafaa kuvaliwa ofisini kwa mtu ambaye hapaendelei kuvaa suruali. Kuna maternity sketi ambazo tumboni kunakuwa na belti kubwa la mpira la kukuwezesha kuvaa bila kupata tabu. Vile vile unaweza kuvaa magauni yenye mikono midogo mizuri au yasiyo na mikono na kisha kuvaa na koti dogo zuri au vijisweta vidogo na kukufanya ukaonekana mrembo na mwenye kupendeza.



Nadhani nitakuwa nimekusaidia, na wengine pia.
Ubarikiwe

Maternity Wear


Muda mrefu hatujaongelea mambo ya urembo na mavazi na leo nimeonelea tuangalie kidogo mavazi mbalimbali yanayopendeza kuvaliwa wakati wa ujauzito. Wengi tumezoea kuvaa nguo kubwa za vitenge zinazofika hadi chini, ni sawa kabisa lakini inapendeza ukiwa unavaa nguo za aina tofauti tofauti ambazo ni nzuri na hazikubani wala kukufanya ukaonekana mkubwa sana.
Hapa kuna baadhi ya nguo ambazo ukizivaa wakati wa ujauzito kwa kweli zinavutia, unaweza ongezea nakshi kama skafu, mtandio au hata kikoti kidogo na wewe mwenyewe ukajisikia vizuri.



NGUO IPI .....???????? IVALIWE WAPI?..................................

 
hebu leo tuongee kuhusu mavazi yetu hasa kina dada,
na hasa mavazi ya ofisini, na pia tuelimishane jamani, ni vazi gani la ofisini??? ni vazi gani la sherehe? ni vazi gani simple tu kwaajili ya nyumbani? na mavazi mengine meeeeeengi, TUTAKUWA TUKIANGALIA VAZI MOJA MOJA, NA LEO TUTAANGALIA JUU YA MAVAZI YA OFISINI TU!
Vazi gani hasa kwa wadada linafaa kuvaliwa ofisini???Tuambie uonavyo wewe
 
Unaweza kuvaa suti yeyote ile na ukapendeza,


si lazima suti tu, unaweza kuvaa hata kiblauzi chako simple skirt or trouser  na ukanoga tu


kama hawa huyu kavaa simple na amenoga, huyu nae suti pia amenoga


but naona kama vile suti zinapendwa sana ofisini,


unaonaeeee, mrembo huyo nimependa sana alivyovaa, BELT linakwenda na SKIRT yake, blauzi inaignia kidogo kwenye hiyo rangi ya skirt, umeona kiatu kileeeeee, (nimekipenda sana) basi pale kwa pembeni unapiga pochi black, We  inanoga hiyo, usipime!!!!!


mh! hapo sasa,!!!!!!!!!! si umeona tofauti iliyopo? si kwamba hajapendeza, kapendeza sana, lakini hii ni yakuvaa ofisini kweli?  sema na wewe, unaonaje? ofisini tuvae vipi wadada??? 
 
 

MAVAZI YA OFISINI

Habari  zenu Wapendwa, tumshukuru Mungu kwa kuiona tena siku hii ya leo, Mpenzi msomaji wa blog hii nakukalibisha kwa mara nyingine tena  usisite kutoa maoni yako  karibu sana.


Siku ya leo nitazungumzia kuhusu Mavazi ya ofisini  ni mavazi ya aina gani? siku ya leo utaweza kuyafahamu kwa undani zaidi , msomaji  mwavazi ya ofisini ni mavazi yanayo heshimika sana  mtu hawezi kuvaa jinzi au  suluali ya jinzi  kwa upande wa wasichana na wanawake hilo sio vazi la ofisini ingawa asilimia kubwa  wana vaa bora  amekwenda ofisini. Lakini ofisini ni sehemu muhimu sana kwa kuvaa vazi la heshima . haya ni baadhi ya mavazi ya ofisini  yanavyo leta muonekano tofauti.
Hili  ni moja wapo ya vazi la ofisini  linalo leta muonekano  tofauti kwa wavaji,pia rangi nyeupe na nyeusi ni moja wapo ya rangi zinazo leta mvuto na inapendeza kwa  kila mtu.




Rangi  ya  Blue na black ni rangi inayovutia sana kwenye mavazi ya suti   wadada wengi wanapenda sana kuvaa aina hii ya rangi.


Tumeweza kuyaona baadhi ya mavazi ya Ofisini yanavyo mfanya mtu awe tofauti hata mtu akivaa vazi la suti akawa anaenda sehemu nyingine tofauti na ofisini,anaonekana tu kama anafanya kazi. Kama tulivyo yaona mavazi ofisini  ni mavazi yanayo heshimiwa sana.





Muonekano tofauti



Mpenzi msomaji hayo yalikuwa ni mavazi ya ofisini, tuangalie upande mwingine wa Viatu pamoja mikoba inayo faa kuvaa kwenye mavazi ya ofisini na kumfanya mvaaji aonekane wa tofauti.


 Kwa upande wa  Viatu


 
inapendeza sana kwenye vazi la suti ukiwa umevaa vazi la black na white inavutia sana




Kwa wale wakinadada na wakina mama wanaoweza kutembelea viatu vya juu kama nilicho kuonesha hapo juu ni moja wapo ya kiatu kinacho pendeza sana , ila kina faa kwa wale wenye magari yao sio unapanda daradara ukiwa umevaa kiutu kama hiki.

Kwa upande wa pochi

  Ni pochi gani inafaa kuvalia nguo za suti












Hizi ni baadhi ya pochi zinazo leta mvuto kwa wanawake na wasichana  na kwa upande wa mavazi ya siti. Mpenzi msomaji wa blog hii utakuwa umeweza kuyaona mavazi ya ofisini pamoja na pochi na  viatu , msomaji endelea kuwa nami katika blog hii karibu sana


 hapo hupo msomaji ina pendeza sana