Bwana Emmanuel Kimaro mwanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha [AJTC],amewahasa wanafunzi wenzake kutumia fursa mbalimbali ili kujipatia ajira na kuachakutegemea kuajiriwa.
Bwana Emmanuel ambaye ni graphics designer ametoa rai hiyo wakati akizungumza na mmiliki wa ukurasa huu mapema leo wakati akiwa chuoni hapo.
Ameongeza kwakusema vijana wengi wawapo chuoni wanategemea ajira hali hii huwafanya kukaa muda mrefu nyumbani baada ya kuhitimu mafunzo chuo,Bila kujua kuwa kupitia elimu waliyopata chuoni wanaweza kuitumia kujipatia ajira.
Nae Bi Neema Ulomi ambaye nimhitimu katika chuo cha ualimu Marangu amekiri kuwa vijana wengi hawajitumi kutafuta fursa kutokana na kutokuwa na malengo.
Bwana Kimaro amehitimisha kwakuwahasa wanafunzi wenzake kuwa na malengo pamoja na kujali muda kwani ndio njia pekee ya wao kutimiza maleongo yao..
No comments:
Post a Comment